Zoezi la kuweka alama ya X kwa nyumba mbazo zipo katika bonde la mto
msimbazi kata ya hananasifu limeanza
leo ambapo tayari nyumba zaidi ya 478
zimewekwa alama hiyo kwa ajili ya kubomolewa .
Wakizungumza
na waandishi wa habari waliofika eneo la msimbazi jijini Dar es salaam wahanga walioathirika na zoezi hilo wametoa malalamiko tofauti juu ya hatua hiyo ambapo wengi wao wamedai kutopatiwa
viwanja mbadala.Aidha muhanga mwingine Elizabeth Masawe amedai kuwa tokea aliponunua kiwanja
hicho eneo hilo lilikuwa halijapimwa.
No comments:
Post a Comment