Tuesday, 29 December 2015

NAIBU katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi, John Mngodo, amelitaka jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa mikakati dhidi ya mauaji ya wazee nchini



NAIBU katibu mkuu  wizara ya mambo ya ndani ya nchi, John Mngodo, amelitaka jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa mikakati dhidi ya mauaji ya wazee nchini.Hayo amesema katika mkutano wa mwaka wa wadau mbalimbali kujadili hali ya ukatili na mauaji ya wazee kwa imani za kishirikina nchini uliofanyika jijini mwanza .Mngodo amesema wananchi wanatakiwa kuwa  tayari kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya kuua wazee kwa kisingizio cha imani za kujihusisha na vitendo vya ushirikina zinazohusisha waganga wa jadi na wapiga ramli.Amesema jeshi la polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali katika
kupambana na tatizo la mauaji ya wazee, ambazo ni ufinyu wa pesa zilizotengwa katika bajeti kwa ajili ya upelelezi, baadhi ya viongozi
na wananchi kuwa waoga wa kutoa taarifa sahihi za wahusika wa kadhia
hiyo.
Juhudi za serikali na wadau mbalimbali zimesaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza mauaji ya wazee kutoka 629 mwaka 2012 hadi 469 kwa mwaka 2014.Naye meneja mradi wa haki ya wazee wa shirika la kimataifa lisilo la kiserikali la Help Age Tanzania, Joseph Mbasha, amesema jeshi la
polisi likishirikiana na wananchi wanaweza kuwatambua wanaofanya
vitendo vya mauaji ya wazee.

No comments:

Post a Comment