Mkurugenzi
wa huduma za mifugo Tanzania Dk Abdi Haygamo
amewatahadharisha wananchi kutojichukulia sheria mkononi ambazo zinasababisha mauaji kwa wakulima na
wafugaji.
Kauli hiyo ameitoa
leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
kuhusiana na madhara yatokanayo na kuchukua sheria mkononi ambapo huleta
madhara makubwa katika jamii ikiwemo kiuchumi.
Aidha amesema kuwa Wizara ya kilimo, mifugo na
uvuvi,imepokea kwa masikitiko mauaji ya
wakulima na wafugaji yaliyotokea hivi karibuni
katika wilaya ya mvomero mkoani morogoro
yaliyosababisha mkulima mmoja
kuuwawa, na watu 4 kujeruhiwa.
Vile vile wizara inatoa pole kwa wote
walioathirika kutokana na mgogoro wa
kijiji cha dihida wilayani mvomero mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment