Saturday 5 December 2015

Father Christmas Afariki Dunia

 Santa
 Father Christmas alifariki akiwa na umri wa miaka 227, kwa mujibu wa tangazo gazeti hilo

 Gazeti moja nchini Norway limelazimika kuomba radhi baada ya kuchapisha tangazo la kicho cha "Father Christmas".
Tangazo hilo lilikuwa la "Mpendwa Father Christmas, aliyezaliwa 12 Desemba 1788", ambaye alidaiwa kufariki tarehe 3 Desemba mjini Nordkapp, ulio kaskazini mwa Norway.
Ibada ya mazishi ilifaa ifanyike 28 Desemba katika kanisa la North Pole Chapel", kwa mujibu wa tangazo hilo.
Gazeti hilo la Aftenposten, ambalo ndilo la pili kwa umaarufu nchini Norway, lilisema kosa hilo lilitokana na taratibu zake za utenda kazi.
"Aftenposten ina taratibu kali kuhusu habari na kutumiwa kwa ishara na mifano katika matangazo yetu ya vifo. Tangazo hili linakiuka taratibu hizi na halikufaa kuchapishwa,” gazeti hilo limesela kupitia taarifa

No comments:

Post a Comment