Tuesday, 8 December 2015

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar pistorius apewa dhamana

 http://cdn.24.co.za/files/Cms/General/d/981/9ed0ed9ab30a462285456550298c34da.jpg

Mahakama kuu mjini pretoria imeipa dhamana  mwanariadha  Oscar Pistorius  huku akisubiri kuhukumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake 2013.
 http://cdn.24.co.za/files/Cms/General/d/1008/1e4f8a970bc74365afe17bfe79518857.jpg
Kikao cha kumhukumu kitaandaliwa Aprili 18 mwaka ujao.
Jaji Aubrey Ledwaba amesema hakuna hatari kwamba Pistorius anaweza kutoroka akipewa dhamana kwani alijiwasilisha mahakamani mwenyewe leo.
 SURROUNDED:
Bw Pistorius, mwenye umri wa miaka 28, ametakiwa kulipa rand 10,000 ($700) kama dhamana.
Ataendelea kutumikia kifungo cha nyumbani na atakuwa na kifaa cha kumfuatilia kielektroniki. Anaruhusiwa kuondoka nyumbani kati ya saa moja asubuhi hadi saa sita mchana katika eneo la nusu kipenyo la kilomita 20 kutoka kwa nyumba anamoishi.
 
Pistorius pia ametakiwa kusalimisha pasipoti yake kwa mahakama.
Anakabiliwa na kifungo cha zaidi ya miaka 15, ingawa jaji huenda akampunguzia hukumu.
Bingwa huyo wa Olimpiki alirejea kortini leo baada ya mahakama ya rufaa kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini wa kumpata na hatia ya kuua bila kukusudia na badala yake ikaagiza ahukumiwe kwa mauaji

No comments:

Post a Comment