Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewataka
wananchi kuwa watulivu na kuendelea kulinda amani iliyopo hasa wakati huu wa
kuelekea katika sikukuu ya mwaka mpya.
Jeshi hilo limesema limeweka
mikakati kuhakikisha wakati
wa mkesha wa mwaka mpya hali ya usalama inakuwa shwari.
Katika taarifa iliyolewa leo ambayo imesainiwa na kamishina wa jeshi
la polisi kanda maalum ya Dar es salam
Suleimani Kova imesema jeshi hilo
limejipanga vizuri katika kulinda
usalama.
Kamanda Suleimani Kova
Imesema vikosi vyote vya jeshi hilo viko vizuri na
pia wana mikakati mbali mbali kwa ajili ya kudumisha amani.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa kikosi cha anga kitafanya doria kwa kutumia
helkopta ya polisi sambamba na askari wa
pikipiki ambao watakuwa na doria katika mitaa mbali mbali.
No comments:
Post a Comment