Imeelezwa Ugonjwa wa kipindu pindu
umepungua kwa asilimia kubwa katika mikoa mbali mbali hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri wa
afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu amesema mikoa ya
Dar es salaam,mwanza ,Arusha na Mbeya imefanikiwa kwa asilimia kubwa kupunguza
kasi ya ugonjwa huo.
amesema jumla
ya mikoa 10, imeathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu ambapo kwa sasa mkoa wa morogoro vijijini,Iramba na Arusha
mjini, ndio halmashauri zinazoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi.
ummy mwalimu.
Kufuatia hali hiyo Watendaji wa halmashauri,waganga
wakuu na wilaya wametakiwa kutoa taarifa
sahihi za kila wiki kuhusu ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment