Monday, 28 December 2015

ZAIDI ya ekari 40 za mazao zimeharibiwa kutokana na mvua kubwa kunyesha katika kijiji cha Buchambaga kata ya Chela wilayani Kahama mkoani Shinyanga.



 














ZAIDI ya ekari 40 za mazao  zimeharibiwa kutokana na mvua kubwa kunyesha  katika kijiji cha Buchambaga kata ya Chela wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari  afisa mtendaji wa kata hiyo, John Mahona, amesema mvua hiyo imeharibu mashamba ya mahindi, maharage, viazi na karanga huku kaya 10 zikiharibiwa nyumba zao na mvua hiyo.
 amesema tayari taratibu za kufikisha maafa hayo wilayani zinafanyika huku mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala akikiri kupokea taarifa ya maafa ya mvua hiyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Elias Saleh, amesema mvua hiyo ilianza kunyesha saa 8 mchana, lakini haikuweza kusababisha madhara kwa watu na mifugo kijiji hapo.
Aidha amewataka wananchi kuchukua  tahadhari  katika msimu huu wa mvua kutokana na taarifa za awali za mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), kusema mwaka huu kuna kiwango kikubwa  cha mvua.



No comments:

Post a Comment