Thursday 3 December 2015

Mahakama kuu ya Afrika kusini imemkuta na hatia mwanariadhaa Oscar pistorius

 Legal Law Court

Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini imempata mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius na hatia ya mauaji.
Mahakama hiyo imekubali rufaa iliwasilishwa na upande wa mashtaka ikitaka Pistorius apatikane na hatia ya mauaji, ambayo adhabu yake ni kali zaidi kuliko ya kuua bila kukusudia.
Jaji Lorimer Leach amesema mwanariadha huyo anafaa kurejeshwa kwa jaji aliyemhukumu ili apokee adhabu ya kosa la mauaji.
Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 2013 baada ya kufyatua risasi kupitia mlango wa choo
 
           Oscar akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp

Oscar amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani baada ya kukaa mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia

No comments:

Post a Comment