Friday 18 December 2015

Muungano wa nchi wanachama wa Afrika Magharibi ECOWAS umeyataka mataifa wanachama wa umoja hu kupiga marufuku mtandio unafunika hadi uso



 
Muungano wa nchi wanachama wa Afrika Magharibi ECOWAS umeyataka mataifa wanachama wa umoja hu  kupiga marufuku mtandio unafunika hadi uso, ili kuzuia mashambulio yanayotekelezwa na wanawake wa kujitoa mhanga.
Makubaliano hayo yametolewa  katika Mkutano wa umoja huo   uliofanyika mjini Abuja Nigeria ambapo  umesema mtandio huo wa hadi uso unayumbisha operesheni za maafisa  usalama katika kuwanasa wahalifu.
Imeelezwa kuwa kaskazini mwa nchi ya  Nigeria wapiganaji wa Boko Haram wamekua wakitumia wasichana wadogo na wanawake kutekeleza mashambulio ya kujitoa mhanga.
 Kundi hilo pia limetumia mbinu hiyo katika mataifa ya Cameroon, Chad na Niger ambayo yanashiriki katika operesheni dhidi ya Boko Haram.

No comments:

Post a Comment