Kikosi cha makomando wa nchini Marekani kilichoenda nchini Libya siku chache zilizopita kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na mawasiliano na jeshi la nchi hiyo kimetakiwa kutoka nchini humo.
Afisa wa Wizara ya Ulinzi nchini Marekani ambaye hakutaka jina lake litajwe amethibitisha kuwa, picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii na jeshi la Libya zikionyesha makomando hao wakiondoka nchini humo, ni za kweli.
Amesema makomando hao walilazimika kuondoka Libya muda mfupi baada ya kuwasili, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kundi moja la waasi katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Kikosi hicho cha makomando wa Marekani kilienda Libya mnamo Disemba 14, kwa kile kilichotajwa kuwa ‘kuimarisha uhusiano wa kiulinzi na kiusalama na jeshi la nchi hiyo
No comments:
Post a Comment