Uamuzi huo umetolewa wiki iliyopita katika mkutano uliofanyika nchini Addis Ababa Ethiopia.
Umoja wa Mataifa unakadiria watu zaidi ya mia nne wameuawa tangu kuanza kwa machafuko hayo mwezi Aprili wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania tena nafasi ya urais kwa muhula wa tatu.
Maafisa wa UN wameonya nchi hiyo kukabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Lakini mauaji mabaya zaidi yametokea Ijumaa ya wiki iliyopita wapiganaji waliposhambulia maeneo ya jeshi Bujumbura na kusababisha watu 87 kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment