Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi watendaji wakuu wa
mfuko wa taifa wa bima ya afya kupisha uchunguzi kuhusu wizi na udanganyifu uliofanywa katika akaunti ya madai ya NHIF mkoa wa Mara.
Taarifa za awali zinaonesha zaidi ya shilingi bilioni 2.9 zimeibwa
kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti yamadai ya NHIF mkoa wa
Mara ambazo zimekuwa zikichukuliwa kidogokidogo kwa kipindi cha miaka
mitatu tangu 2013.
Waliosimamishwa ni kaimu mkurugenzi mkuu Michael Mhando, mkurugenzi
wa fedha na vitega uchumi Deusdedit Rutaza, mkurugenzi wa mifumo habari
Ally Othman na mkaguzi mkuu wa ndani Anne Maneno.
Waziri Ummy Mwalimu pia ameagiza mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu
za serikali kufanya uchunguzi maalum wa mfumo mzima wa utoaji madai wa
NHIF pamoja na akaunti zake katika mikoa yote ili kubaini ukubwa wa
tatizo na hatua kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment