Thursday, 21 April 2016

Muongozaji wa Filamu za James Bond afariki Dunia

 
Mwelekezi wa filamu ya James Bond Guy Hamilton amefariki akiwa na umri wa miaka 93.

Aliyekuwa nyota wa filamu hiyo ya 007 Roger Moore alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba alihuzunishwa na kifo chake.
Hamilton alimuelekeza Roger Moore katika filamu ya Live and Let Die pamoja na The man with the Golden Gun.
Pia alifanya uelekezaji katika filamu za Sean Connery in GoldFinger na Diamond are Forever.
Hospitali moja katika kisiwa cha Uhispania cha Majorca ,ambapo Hamilton aliishi ilithibitisha kwa chombo cha habari cha AP kwamba amefariki sikju ya Jumatano.
Filamu nyengine zilizoelekezwa na Hamilton ni pamoja na The Battle in Britain,Force 10 from Navarone,Evil under the sun na The Mirror Crack'd.

No comments:

Post a Comment