Thursday, 21 April 2016

Farid Mussa kuelekea Hispania kesho kwa majaribio



Kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kuwasili kesho kikitokea nchini Tunisia ambapo wamemuacha winga chipukizi wa Klabu hiyo Farid Mussa ambaye kesho anatarajia kuelekea nchini Uhispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Afisa habari wa Azan FC Jaffery Iddy Maganga amesema, Farid atakuwa huko kwa takribani mwezi mmoja na atafanya majaribio katika timu za Malaga na Las Palmas zinazoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo na atarejea jijini Dara es Salaam Mei 19 mwaka huu msimu wa ligi ukiwa umeisha.
Maganga amesema, kwa upande wa kikosi cha Azam kitakachowasili kutokea nchini Dubai ambapo kilipitia kikitokea nchini Tunisia hakitaingia kambini bali kitaunganisha safari kuelekea jijini Mwanza ambapo kitapumzika kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho Tanzania Bara dhidi ya Mwadui ya mjini Shinyanga utakaopigwa Aprili 24 mwaka huu mjini Shinyanga.
Maganga amesema, kwa upande wa kocha wa kikosi hicho Stewart Hall mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ratiba jinsi ilivyopangwa lakini kikosi kimeshaandaliwa kwa ajili ya kuweza kufanya vizuri katika mchezo huo.
Azam FC itakuwa ugenini dhidi ya Mwadui huku Yanga ikiwa pia ugenini Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ikicheza dhidi ya Coastal Union.

No comments:

Post a Comment