Thursday, 21 April 2016

Uchaguzi wa viongozi TSCA kufanyika Mei 21 mwaka huu

Chama cha Makocha wa Mchezo wa kuogelea nchini Tanzania TSCA kinatarajia kufanya uchaguzi wake Mei 21 mwaka huu jijini Dasr es salaam.
Rais wa TSCA Alexander Mwaipasi amesema, uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika mwaka jana na walitangaza nafasi lakini watu hawakuweza kujitokeza kwa ajili ya klugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.
Mwaipasi amesema, viongozi hao waliopo hivi sasa wameshamaliza muda wao tangia mwaka jana kwa mujibu wa katiba hivyo wamejiandaa ili kuweza kufanya uchaguzi na kuweza kupata viongozi watakaoendeleza chama hicho.
Nafasi zitakazowaniwa katika uchaguzi huo ni nafasi ya Rais, Katibu mkuu, Katibu Mkuu msaidizi, Mkurugenzi wa fedha, Mkurugenzi wa ufundi, Mkurugenzi wa fedha msaidizi na Mkurugenzi wa habari na uenezi ambazo fomu na Baraza la michezo nchini BMT.

No comments:

Post a Comment