Thursday, 21 April 2016

Simba kuelekea Zanzibar kesho maandalizi dhidi ya Azam FC

Kikosi cha Simba SC kinatarajia kuelekea visiwani Zanzibar hapo kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa Mei 1 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Meneja wa Simba SC Abbas Ally amesema, wanaamini kambi hiyo itaweza kuwasaidia kupata pointi tatu katika mchezo huo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.
Abbas amesema, kambi hiyo itakuwa ya muda mfupi lakini wanaamini wataweza kufanya vizuri katika mchezo huo ambao kwa upande wao ni muhimu kwa ajili ya kuweza kurudisha imani za mashabiki wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment