Thursday 21 April 2016

Mganga Mkuu wa Serikali:Asilimia 25 ya Watanzania ni wagonjwa

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari amesema kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwani Takwimu zinaonyesha asilimia 20 mpaka 25 ya watanzania wana magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na magonjwa ya Moyo, Kisukari na Kansa.

Profesa Bakari ametoa kauli hiyo hii leo alipokuwa akifungua Mkutano wa kimataifa wa Madaktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wenye lengo la kujadili namna ya kuisaidia Serikali katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Aidha serikali kwa hivi sasa inaandaa mazingira ya kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujizuia kupata maradhi haya kwani ni vigumu sana kutibu maradhi haya kuliko kuyazuia na yanahitaji rasilimali kubwa ili mtu aweze kupata nafuu.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete Mohamed Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kupunguza nusu ya wagonjwa waliokuwa wanasafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya upasuaji wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambapo kwa mwaka jana pekee wamefanya upasuaji wagonjwa 648 na wanatarajia kwa mwaka huu watafanya upasuaji kwa wagonjwa wengi zaidi ambapo kwa kipindi cha miezi 3 wameshawafanyia upasuaji wagonjwa 230.

No comments:

Post a Comment