Friday 22 April 2016

Kauli ya Rais John Magufuli kuhusu Wezi,na mafisadi nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kwa watu wote ambao wamewaibia wananchi watatajwa hadharani kama wao walivyo waibia wananchi hadharani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipokuwa akiwahutubia wenyeviti na makatibu wa CCM kutoka mikoa yote Tanzania
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wenyeviti, makatibu wa Chama cha Mapinduzi wa mikoa na wilaya za Tanzania bara na Visiwani Ikulu jijini Dar es Salaam.
''Mnawaibia watanzania halafu mnalalamika haki za binadamu ninapowatumbua na kuwatangaza hadharani, nitaendelea kuwatumbua na ninyi mpate uchungu mliowasababishia watanzania maskini''

''Kwa hiyo ninyi mlikuwa mna haki kuwaibia hadharani watanzania? Mmewaibia watanzania hadharani, ni lazima tuwatangaze hadharani, hata hao wanaowatetea kwa kisingizio cha haki za binadamu naona nao ni majipu na tutaanza kuwafuatilia''.
Rais pia amewataka viongozi wote ambao wapo chini ya uteuzi wake kufanya kazi kwa uadilifu kwani watakao haribu au kuwaibia watanzania atawatangaza hadharani kama alivyowatangaza siku ya uteuzi.
''Kwa nini mfurahie kutajwa hadharani siku ya kuteuliwa lakini msitajwe hadharani siku ya kutumbuliwa? Ukibainika umeiba hakuna muda wa kujieleza kwa sababu haukujieleza wakati unawaibia wananchi maskini."----Rais John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment