Friday, 22 April 2016

Raisi Magufuli atoa idadi ya wafanyakazi hewa nchini


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia jana wafanyakazi hewa waliobainika na kutolewa katika malipo waliyokuwa wakiyapata kama mshahara na posho nyingine wamefikia 7700.

Akizungumza Jana Ikulu Jijini Dar es Salaam na Wenyeviti na Makatibu wa CCM, nchi nzima, rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema idadi hiyo ni mpaka kufikia siku ya jana lakini bado uchambuzi unaendelea ili kubainia wafanyakazi hewa wengi zaidi.
Rai sDkt. Magufuli amesema kuwa mabilioni ya fedha yaliyokuwa yanapotelewa kwa watu wachache yangeweza kuboresha huduma za kijamii nchini na yangeweza kuepusha vifo ambavyo havikuwa vya lazima.
Dkt. Magufuli amesema kuwa kupotea kwa fedha hizo kumepunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kutokana na fedha hizo zingeweza kutumika kununua madawa Hospitalini, Ujenzi wa Madarasa, Madawati na vitu vingine.

No comments:

Post a Comment