Saturday, 23 April 2016

Kauli ya Serikali kuhusu bunge kurushwa LIVE

 






Serikali imeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni kufuata taratibu wakati wa kuwasilisha madai yao na sio kususia mijadala mbalimbali inayoendelea bungeni.

Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye ametoa kauli hiyo Bungeni Dodoma baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kudai kuwa taratibu zimekiukwa kwa wananchi kukosa kufuatilia matangazo ya Bunge na hivyo kutishia kususia kuchangia bungeni na kuangalia hatua zipi watachukua
Kauli hiyo ya Waziri Nape imeungwa mkono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Januari Makamba.
Jana akizungumza na waandishi wa Habari Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Freeman Mbowe alisema kuwa hawatakubali kutishiwa ili wawe wapole na kutoonyesha Bunge ni kuwanyima wananchi fursa ya kupata habari.
''Waziri Mkuu wa Nchi anawasilisha malengo ya serikali na duniani huko wananchi hawajui nini kinaendelea 'this is not fair'''-Freeman Mbowe.

No comments:

Post a Comment