Friday 29 April 2016

Kauli ya Tanesco kuhusu watumiaji wa vifaa bandia


Watumiaji wakubwa wa umeme wametahadharishwa kuhusu vifaa vingi bandia vya umeme vinavyoingizwa kwa wingi hapa nchini, hali inayoweza kuwasababishia hasara kubwa na hata maafa.

Tahadhari hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ABB inayohusika na vifaa vikubwa vya umeme katika mkutano wa siku mbili na wadau wa umeme uliondaliwa na kampuni hiyo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu teknolojia mbalimbali za umeme.

Amesema vifaa bandia vya umeme ndiyo imekuwa changamoto kubwa katika sekta ya nishati hapa nchini, ambapo ametoa wito kwa watumiaji wa vifaa vikubwa vya umeme kuhakikishia wanatumia vifaa halisi.

Kampuni ya ABB inazalisha na kusambaza vifaa vizito vya umeme na wateja wake ni mashirika makubwa yanayotumia umeme mwingi ikiwemo Tanesco.

No comments:

Post a Comment