Friday, 29 April 2016

Kauli ya TCRA kuhusu taarifa za Uhakiki wa Simu bandia hii hapa



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewakumbusha watumiaji wote wa simu za mkononi nchini kuhakikisha kwamba simu zao zimehakikiwa ili kuepuka usumbufu utakaoweza kutokea wakati wa kipindi cha mpito cha uhakiki wa simu kitakapomalizika Juni 16 mwaka huu.

Aidha,Mamlaka hiyo imewakumbusha wauzaji wote wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kuwa ni kosa kisheria kubadilisha namba tambulishi ya vifaa hivyo na adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 10 au faini isiyopungua Shilingi Milioni 30 au vyote ka pamoja.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania Mhandisi James Kilaba amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwamba Mamlaka hiyo inaendelea na zoezi la kuelimisha umma kuhusu ukomo wa matumizi ya simu bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu.

Akitoa tathmini ya hali halisi kuelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini ifikapo Juni 16 mwaka huu, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka yake imekumbana na changamoto kadhaa.

No comments:

Post a Comment