Friday, 29 April 2016

Utafiti mpya kuhusu ajali barabarani na pikipiki huu hapa

 
Utafiti umeonesha kuwa asilimia 80 ya majeruhi wa ajali za barabarani wanatokana na ajali za pikipiki na kwamba waathirika wamekuwa wakijeruhiwa kichwani kutokana na mazoea ya kutovaa kofia ngumu hasa kwa wafanyabiashara wa usafiri huo maarufu kama bodaboda. 

Katika mkutano wa wadau mbalimbali wa usalama barabara wenye lengo la kutengeneza mkakati wa pamoja wa kupunguza ajali za barabarani mkoani Shinyanga, inaelezwa kukosa ushirikiano kwa wadau mbalimbali hasa taasisi za serikali kumesababisha watu kupoteza uhai.

Amesema changamoto hiyo ya kupunguza ajali itafanikiwa iwapo idara nyingine za serikali zitatimiza wajibu wake.

No comments:

Post a Comment