Friday 15 April 2016

Liverpool ya staajabisha ulimwengu(Full Time,uchambuzi,picha)

 The Kop pays tribute to the 96 supporters who died at Hillsbrough on the eve of the 27th anniversary of the disaster
Majogoo wa jiji’ Liverpool wameushangaza ulimwengu kwa mara nyingine tena baada ya kutoka nyuma ya Borussia Dortmund na kufanikiwa kushinda game kwenye uwanja wa Anfield kisha kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa League.

Kikosi cha Jurgen Klopp walifungwa magoli mawili ya fasta na kutakiwa kuhitaji kuifunga Dortmund magoli matatu ili kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Lakini vidume walipambana na kuupanda mlima huo kabla ya Dejan Lovren aliyetokea majeruhi kusukuma kambani krosi ya James Milner kambani na kuihakikishia ushindi timu yake.

Liverpool 4-3 Borussia Dortmund (5-4 agg): Dejan Lovren, Mamadou Sakho, Phillipe Coutinho
Wakiadhimisha kumbukumbu ya miaka 27 ya janga la ‘Hillsborough’ ambapo takribani mashabiki 96 walifariki dunia kwenye dimba la Anfield, uwanja mzima ulisimama kutoa heshima kwa mashabiki hao kwa dakika moja kabla ya game kuanza ambayo itakumbukwa vizazi na vizazi vya mashabiki wa Liverpool.
Doertmund walipata magoli mawili ndani ya dakika tisa za kwanza kupitia kwa Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang na kuwa mbele kwa aggregate ya magoli 3-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Signal Iduna Park, Ujerumani juma lililopita.
Miamba hiyo ya Bundesliga ilipoteza nafasi nyingi za kufunga na kuongeza gape kubwa la magoli kati yao na Liverpool kabla ya wekundu hao wa Anfield hawajarejea kwenye mchezo kwa mashambulizi ya aina yake.
Taratibu Liverpool ikaanza kurudi mchezoni kwa kutengeneza na kupoteza nafasi kadhaa. Na baada ya Divock Origi kuwapa 
 Origi grabbed the ball out of the night and encouraged more noise from the Liverpool fans after scoring in the second half
                    origi akishangilia goli la kwanza
matumaini kwa kuzifungua nyavu za Dortmund dakika za mapema kipindi cha pili akiupitisha mpira katikati ya miguu ya golikipa Roman Weidenfeller lakini bado walidhoofishwa na goli la tatu la Marco Reus lililofungwa dakika ya 57 kwa mkwaju mkali takribani mita 14 toka golini.
Liverpool ilihitaji magoli matatu sasa ili kufuzu kwa hatua inayofuata, zikiwa zimesalia dakika 25 pambano kumalizika, Philippe Coutinho alipachika bao la pili kabla ya Mamadou Sakho kuongeza bao la tatu dakika ya 77 na kufufua matumaini ya uwezekano wa Liverpool kusonga mbele.
Alikuwa ni Lovren ambaye aliibua shangwe za mashabiki wa Liverpool dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kupiga bao lililoipa Liverpool ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Dortmund na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya Europa League.
 Central defender Lovren (centre) had the last say, heading in strongly at the back post to send Liverpool into the last four
               lovren akiifungia liverpool goli la nne


Liverpool: Mignolet, Clyne, Lovren, Sakho, Moreno, Lallana (Allen, 62), Milner, Can (Lucas, 81), Coutinho, Firmino (Sturridge, 62), Origi. 
Subs not used: Ward, Skrtel, Smith, Ojo.
Goals: Origi 48, 
Coutinho 66, 
Sakho, 77
 Lovren, 91.

Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Papastathopoulos, Hummels, Schmelzer, Mkhitaryan, Castro (Ramos, 82), Weigl, Reus (Gundogan, 82), Kagawa, Aubameyang. 
Subs not used: Burki, Bender, Sahin, Pulisic, Ginter.
Goals: 
Mkhitaryan 5, 
Aubameyang 9, 
Reus 57. 

Referee: Cuneyt Caki


Timu zilizoingia nusu fainali ya EUOPA LEAGUE 

Liverpool
Sevilla
Shakhtar Donetsk
Villarreal

No comments:

Post a Comment