Thursday 14 April 2016

Mkutano wa Wadau wa maendeleo na sekta binafsi wamekutana leo jijini Dar es salaam

IMG_5293
Wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi wamekutana leo jijini dar es salaam ili kujadiliana ni jinsi sekta binafsi inavyoweza kuchangia katika malengo 17 endelevu ya milenia SDG.

Akifungua mkutano huo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema awali serikali ilikuwa ikitekeleza malengo ya milenia peke yake bila kushirikisha sekta binafsi jambo ambalo kwa sasa litakuwa ni tofauti.
Amesema katika kuelekea kwenye malengo endelevu ya milenia ni muhimu sasa serikali, taasisi mbalimbali pamoja na sekta binafsi zikashirikiana ili kutekeleza kwa haraka malengo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu kutoka taasisi ya African Sustainable Business bwana Raymond Mubayiwa ambao ndio waandaji wa mkutano huo amesema ni mara ya kwanza mkutano huo kufanyika lengo likiwa ni kuwakutanisha wadau hao kujadiliana na kuona jinsi sekta binafsi inavyoweza kutoa mchango katika utekelezaji wa malengo ya milenia SDG.

No comments:

Post a Comment