Friday, 22 April 2016

Mpango mpya wa kunusuru kaya maskini Tanzania Bil.300 kutumika

Mkurugenzi mkazi wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Alvaro Rodriguez Aakizungumza na wanakijiji wa Mwanabweto
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limesema mpango wa serikali wa kusaidia Kaya masikini nchini Tanzania awamu ya tatu haujawafikia walengwa ambao ni wazee na wanawake ili kuondokana na umasikini uliokithiri katika ngazi ya kaya katika maeneo ya vijijini nchini.
Akizungumza na EATV Mkurugenzi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF Ladslaus Mwamanga amesema Serikali ya Tanzania imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 300 katika kipindi cha Miezi 18,kuwafikia wakazi waliopo katika vijiji 9,980 vilivyopo katika Halmashauri zote 159 za Tanzania bara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kusaidia jamii wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF Amadeus Kamagenge Mpango wa kuzinusuru kaya masikini nchini Tanzania ambazo ni asilimia 28.2 ya watu wote nchini huku asilimia 9.7 wakiwa ni wale wenye umasikini unaoambataña na ukosefu wa chakula.
Zaidi ya shilingi Bilioni 4.5 zimetolewa mwaka Jana katika mkoa wa Pwani,Wazee wa vijiji vya Vikuge na Mwanabwito wilaya ya kibaha mkoani Pwani wanasema fedha wanazopewa kila baada ya miezi miwili haziwatoshi kujikimu.
Amadeus Kamagenge ameongeza kuwa vigezo vinavyotumika kuwapata wanufaika wa mpango huo ni pamoja na kuorodhesha kaya masikini katika kijiji,harafu mkutano wa Wanakijiji unaamua endapo walioorodheshwa kama ni masikini ndio wanaanza kuwagawia fedha za radi huo.
Mtendaji wa kijiji cha Vikuge kilichopo katika mkoa huo,Betram Mfalamagoha amesema utaratibu uliotumika kuwapata masikini walengwa wa mpango huo,umesababisha kuwanufaisha vijana wenye uwezo na sio makini hasa wenye kipato duni na wasiojiweza kama ilivyokuwa malengo ya mradi huo
Kufuatia hali hiyo,Mkurugenzi mkazi wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Alvaro Rodriguez analazimika kuiomba serikali ihakiki upya malalamiko ya mpango huo kuwanufaisha wasio walengwa.
Zaidi ya Shilingi Bilioni 300 zimetumika katika vijiji 9,980 katika mpango huo wa kuzinusuru kaya masikini nchini.

No comments:

Post a Comment