Monday 18 April 2016

Mvua zinazoendelea nchini za sababisha haya Mbeya



Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mbeya, Dk Thea Ntara amesema bado hali ni tete kwa wananchi wa  Kata 10 zilizokumbwa na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha na ameamuru shule tatu za sekondari  na saba za msingi zifungwe kwa  muda usiojulikana baada ya vyumba vya madarasa kujaa maji na miundombinu yake kutishia usalama.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Ntara alisema hali iliyopo si shwari na inaleta hofu ya wananchi wa kata za Makwale, Kajunjumele, Ndogo, Ipinda,Lusungo, Bujonde, Katumba Songwe, Mwaya na Ikama  kutokana na kukosa mahali pa kuishi na Serikali imechukua jukumu la kuwahifadhi kwenye makanisa na katika kambi mbili tofauti zilizopo tarafa ya Unyakyusa na Ntebela na wengine wakichukuliwa na ndugu zao ambao hawajafikwa na maafa hayo.

No comments:

Post a Comment