Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema
kushuka kwa pato la utalii katika Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro
kumechangiwa na wafugaji kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi na
kusababisha kushuka kwa hiyo thamani ya wanyamapori na hifadhi.
Waziri MAGHEMBE amesema hayo katika mahojiano maalumu na Shirika la
Utangazaji Tanzania ambapona ametoa siku thelathini kwa mifugo yote toka
nje ya nchi kurejeshwa makwao na baada ya muda huo mifugo hiyo
itataifishwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri MAGHEMBE pia amesema serikali inafanya tathmini ya biashara ya
wanyama hai ili kudhibiti usafirishwaji wa wanyama hao kinyume cha
sheria.
Katika hatua nyingine waziri MAGHEMBE amewatahadharisha wafugaji
kuepuka kuchanganya mifugo yao na wanyama pori ili kuepuka magonjwa
yanayoweza kusambazwa kutoka kwa wanyama pori kwenda kwa binadamu.
Aidha ameitaka Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi
kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafugaji ili kudhibiti tatizo la
uvamizi wa maeneo ya hifadhi
No comments:
Post a Comment