Sunday 17 April 2016

Tazama Athali ya mvua zinazoendelea jijini Dar es Salaam


Baadhi ya wakazi na watumiaji barabara ya Tabata kisiwani wameulalamikia uongozi wa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam kwa kutoboresha miundombinu ya daraja lililoko katika barabara hiyo na kusababisha adha kubwa wakati mvua inaponyesha.

 katika barabara hiyo ya Tabata kisiwani maji yamefurika na kusababisha kufunikwa kwa  baadhi ya madaraja.
 tbt

Baadhi ya wakazi na watumiaji wa barabara ya tabata kisiwani wamedai kuwa tatizo hilo ni la muda mrefu na limekuwa likijirudia mara kwa mara mvua zinaponyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya upande mmoja na mwingine wa barabara hiyo, jambo ambalo linasababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Jiji la Dar es salaam bado linakabiliwa na ubovu wa miundombinu ya barabara ambapo unasababisha wananchi kupata adha kubwa

No comments:

Post a Comment