Sunday 17 April 2016

Wananchi Vijibweni Kigamboni wafurahishwa na kukamilika Daraja la Kigamboni,

http://i1.wp.com/habarikwanza.com/wp-content/uploads/2015/11/5ccb72ed-d625-46e8-a08a-18eb90da898b.jpg
Wananchi wa VIJIBWENI KIGAMBONI jijini DAR ES SALAAM,wamefurahishwa na kukamilika kwa daraja linalounganisha kitongoji hicho na maeneo mengine mkoani Dar es salaam na kueleza kuwa ni ukombozi mkubwa kwao kutokana na kuwaletea unafuu mkubwa wa nauli kwa watu wa kipato cha chini.

 Furaha hiyo waliitoa leo walipohojiwa na CHANNEL TEN wakati waandishi wa kituo hicho walipofika katika daraja hilo kuona mwitikio wa wananchi walipoelezwa kupitia taarifa ya serikali kuwa, daraja hilo kwa siku ya leo wanaruhusiwa kuvuka bila ya kulipia vyombo vyao vya usafiri kabla halijazinduliwa rasmi , siku ya jumanne na rais Dk. JOHN POMBE MAGUFULI.
 
Hata hivyo baadhi ya wananchi wameelezea upungufu wa baadhi ya miundombinu katika daraja hilo ambapo wamesema suala la vivukio katika mitaro ya maji machafu kutoka upande mmoja kwenda mwingine hauna vifaa hivyo, na mfereji ni mpana na kusababisha wananchi kuzunguuka sana ili wafike upande mwingine wa barabara, ambapo wameomba hilo lifanyiwe kazi.

No comments:

Post a Comment