Friday 22 April 2016

TFDA yakamata shehena ya Vipodozi vyenye Sumu Kariakoo jijini Dar es salaam

 
Mamlaka ya Chakula na dawa -TFDA imekamata shehena kubwa ya vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu hapa nchini.

Shehena hiyo ya vipodozi iliyokutwa kwenye majengo mawili ya ghorofa zilizopo mtaa wa Jangwani kariakoo jijini Dar es salaam,  yalikamatwa na maafisa wa TFDA na kulazimika kuchukua bidhaa hizo baada ya wahusika kukimbia.
Ilichukua saa kadhaa kwa mamlaka ya chakula na dawa kukusanya vipodozi hivyo ambavyo vina viambata vyenye sumu ambavyo vilikuwa vimefichwa kwenye store tofauti ambazo nyingine zilikuwa hazina hata madirisha wala taa, huku ulinzi mkali wa polisi ukiimarishwa ili kuhakikisha mzigo huo unaondolewa kwa usalama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa-TFDA HIITI SILO ameiambia channel ten tangu operesheni za mamlaka hiyo kukabiliana na vipodozi bandia na vyenye viambata vya sumu, hawajawahi kukamata shehena kubwa ya aina hiyo ya vipodozi.

No comments:

Post a Comment