Friday 22 April 2016

Tamko la CUF kuhusu serikali kuzuia Bungeni hii hapa

 Chama cha wananchi Cuf kimelaani hatua ya serikali kuzuia vyombo vya habari kupata habari moja kwa moja kutoka kwenye vikao vya bunge.


 Na kuitaka serikali kupitia Bunge la jamhuri ya Muungano kupitia Upya Sheria na tataribu za kuvibana Vyombo vya habari kurusha au kupata habari moja kwa moja katika vikao vya bunge linaloendelea mjini dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Naibu Mkurugenzi wa habari na Uenezi wa Chama cha wananchi Cuf Abdul Kambaya amesema kitendo cha kuzuia waandishi wa habari kinatafsiliwa kuwa ni dalili za  Udikteta dhidi ya Uhuru wa habari .
Aidha kuvibana vyombo habari kunakiuka katiba ya nchi ya kuwanyima wananchi kupata habari kwa kina kuhusu mjadala wa bunge hasa katika kipindi hiki cha Bunge la bajeti lakini pia wananchi watakosa fursa ya kuchambua majadiliano yanayojadiliwa bungeni kwa ajili ya maendeleo yao.
Amesema kutokana na bunge kuamua kurekodi matukio ya bunge na kuyasambaza katika vyombo vya habari basi hakuna sababu ya waandishi kuhudhuria katika vikao hivyo kwa kuwa taarifa zinazotolewa zinakuwa zinachujwa na kuondoa dhana nzima ya demokrasia ya habari nchini.

No comments:

Post a Comment