Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imesogeza mbele hadi Aprili 27 mwaka huu uamuzi wa hukumu ya kuliondoa shitaka la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapatao Tanzania (TRA)
Kamishna MkuuHarry Kitilya na wenzake wawili Shose Sinare na Sioi Solomoni.
Akitoa taarifa ya kusogezwa mbele uamuzi huo, hakimu Emilious Mchauru amesema Mahakama imeamua kusogeza mbele uamuzi wa kufuta shitaka hilo kutokana na kutokamilika uandikaji wa uamuzi huo baada ya hakimu kukabiliwa na Majukumu mengi ya kikazi.
Amesema watuhumiwa hao watatu sasa watarudishwa Rumande kwa ajili ya kuendelea kusubiria hukumu ya shitaka hilo hadi April 27 ambalo walilifungua Aprili 8 mwaka huu kupitia mawakili wa upande wa utetezi akiwemo Majura Magafu pamoja na Dk Ringo Tenga.
Bwana Harry Kitilya na wenzake wanakabiliwa na Mashtaka nane likiwamo la utakatishaji fedha ambazo ni dola za kimarekani Milioni sita Mali ya Serikali.
No comments:
Post a Comment