Friday, 22 April 2016

TGNP ya wataka wananchi Mbeya kuacha mila kandamizi katika jamii

Wananchi wilayani Mbeya wametakiwa kuachana na mila zinazowakandamiza wanawake kutoa maamuzi kwenye familia kwani kufanya hivyo ni kikwazo cha maendeleo kwenye jamii nyingi hususani vijijini.
Baadhi ya Wanawake Mkoani Mbeya wakiwa katika semina
Hayo yamezungumzwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Mbeya, Zena Kapama, ambapo amesema baadhi ya jamii zimekuwa zikishikilia mila na desturi ambazo zinamnyima mwanamke haki ya kutoa maamuzi kwenye familia zao.
Kupitia Mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) wanawake wa kata ya Igale, Wilayani humo walilalamikia vitendo vya waume zao kuwafanyisha kazi kwenye mashamba na wakati wa mavuno wanayauza bila kuwashirikisha, hali iliyopelekea Afisa Maendeleo ya Jamii kukemea kitendo hicho na kuiomba jamii kuachana na mila hizo.
Kapama amesema kuwa serikali imeendelea kufanya juhudi ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu unyanyasaji wa watoto hali iliyopelekea jamii nyingi kuelimika na kuachana na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment