Mkurugenzi
Mkuu wa TBL GROUP Roberto Jarrin (wapili kushoto) Rais wa shirikisho
la Mpira wa Miguu Nchini (TFF)
Jamal Malinzi (wa pili kutoka kulia) Katibu Mkuu shirikisho hilo ,
Mwesigwa Selestine (kulia) na Mjumbe wa Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa
(kushoto )wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati
walipotembelea katika ofisi za TBL Masaki jijini
Dar es Salaam.
RAIS
wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongoza ujumbe wa
maofisa wengine wawili wa shirikisho hilo wamefanya ziara makao makuu ya ofisi
za TBL Group zilizopo Masaki jijini ambapo walikutana na mkurugenzi wake Mkuu
Roberto Jarrin na kufanya naye mazungumzo.
Ziara
hiyo imeelezwa kuwa ina lengo la kudumisha uhusiano miongoni mwa taasisi hizo
mbili hususani katika kuendeleza mchezo wa soka nchini.
Rais wa
shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kulia )
Katibu Mkuu shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine (kushoto) na Mjumbe
wa Kamati ya TFF Richard Sinamtwa (katikati) wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Roberto Jarrin (Kulia ) wakati walipofanya
ziara ya kikazi ofisini kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP Roberto Jarrin (katikati akisalimiana na Mjumbe wa
Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa , Kulia ni
Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi
No comments:
Post a Comment