Msafara wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo umepotea njia wakati wanaelekea kwenye shule ya msingi Nzuguni B, waziri huyo alikuwa na ratiba ya kufanya ziara ya kutembelea shuleni hapo leo asubuhi kujionea matatizo yanayoikabili shule hiyo.
Msafara huo wa Naibu Waziri ulikuwa unaongozwa na wenyeji wake ambao ni watumishi wa manispaa ya Dodoma ambao walikuwa hawalitambui vizuri eneo hilo walilokuwa wanaenda kulitembelea.
Aidha shule hiyo ya Nzuguni B, haijawahi kutembelewa na ofisa elimu tangu mwaka 2007 licha kuwa shule hiyo ipo umbali wa kilomita sita tu kutoka katikati ya mji wa Dodoma.
Kutokana na kitendo hiko kutomfurahisha, Naibu Waziri alisema, “Mstahiki Meya, mimi niliona wazi kuwa watumishi wako wananipoteza,”
“Nimechukia sana na hawa watu. Tatizo lao ni kwamba hawajawahi kuja katika shule hii tangu mwaka 2007, lakini wamekaa ofisini tu. Ikiwezekana waondolewe na kupelekwa vijijini,” aliongezea waziri Jafo.
No comments:
Post a Comment