Kampuni ya reli nchini,TRL,imeongeza safari za treni ya jiji la DAR ES SALAAM inayofanya safari zake kati ya stesheni maeneo ya MNAZI MMOJA hadi UBUNGO MAZIWA,
kutoka safari sita kwa siku hadi safari nane kwa siku kuanzia kesho jumatatu.
Afisa uhusiano wa kampuni hiyo,MIDLAJ MAEZ,akiongea kwa niaba ya kaimu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya TRL,MASANJA KADOGOSA,amesema lengo la kampuni hiyo ni kuwarahishia wasafiri uharaka wa kufika maeneo ya kazi na nyumbani haraka na kwa bei nafuu.
Amesema kutokana na kampuni hiyo kuwa na uhakika wa kuwa na vichwa vya treni ambavyo ni vipya,uhakika wa huduma hiyo umekuwa ni mkubwa mno hivyo amewaomba watumiaji wa treni hiyo kuitumia kikamilifu ili kurahisisha shughuli zao za kiuchumi na jamii.
Aidha amesema wamebadilisha ratiba ya kituo cha KAMATA kwa kuhakikisha sasa treni inayotoka mjini majira ya saa kumi na mbili jioni inasimama katika kituo hicho tofauti na alivyokuwa awali ambapo ilisimama mara moja wakati inaenda stesheni na wakati wa kurudi haisimami
No comments:
Post a Comment