Sunday, 24 April 2016

Wakazi wa Liwale mkoani Lindi walalamika TANROAD

  Abiria wanaosafiri katika barabara kuu ya Nachingwea Liwale Mkoani Lindi wameomba wakala wa Barabara Nchini

(TANROAD) Mkoani humo kutatua changamoto ya ubovu wa barabara kati ya Wilaya hizo mbili ikiwemo pia barabara ya Liwale – Nangurukuru – Dar es Salaam ili kutoifanya wilaya ya Liwale kuwa kisiwani hali inayochangia kupanda kwa gharama za maisha.
Wakazi hao wameeleza kuwa ubovu wa barabara kuu zinazoelekea wilaya ya Liwale licha ya kuzoretesha uchumi wa wilaya hiyo pia kunasababisha tatizo la usafiri, hali inayowafanya wakazi hao kupata shida kutokana na wamiliki wa magari kupandisha nauli na wakati mwingine kusitisha huduma za usafirishaji hali inapokuwa mbaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Liwale, Gaudence Nyamwihura akizungumzia ubovu wa barabara za kuunganisha wilaya hiyo na maeneo mengine alikuwa na haya ya Kusema Huku akibainisha Jitihada zinazofanywa
Barabara ya kuunganisha wilaya hiyo na wilaya ya Nachingwea yenye urefu wa kilomita 128 pamoja na ile ya Liwale Nangurukuru wilayani Kilwa yenye urefu wa kilometa 231 kwa sasa zinapitika kwa shida kutokana na kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

No comments:

Post a Comment