Sunday 17 April 2016

Wakulima wa zao la Korosho watahadharishwa Ugonjwa Mnyauko unao shambulia Mikorosho,

 
Wakati wakulima wa zao la korosho nchini wakipalilia mashamba yao katika msimu mpya wa kilimo,taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele kwa kushirikiana na bodi ya korosho nchini imewatahadhalisha wakulima kuepuka kusambaza ugonjwa wa mnyauko wa mikorosho unaenezwa kwa kuhamisha udongo kutoka shamba lililoathirika.

 cashew-fruit
Ugonjwa huo ambao ulifahamika kwa mara ya kwanza mwaka 2012 katika kijiji cha Magawa wilayani Mkuranga mkoani Pwani na mwaka 2015 ukaonekana katika wilaya za masasi na tandahimba mkoani Mtwara unakausha majani ya mikorosho na kuadhili uzalishaji .

Mtafiti elekezi wa zao la korosho barani Afrika Profesa Peter Masawe pamoja na mtafiti mstaafu wa taasisi ya kilimo Naliendele Dk. Shamte Shomari wamesema ugonjwa huo ambao chanzo chake kimebainika na unaenezwa kwa kuhamisha udongo huku mikorosho iliyoathirika inakuwa na majani ya rangi ya kahawia na njano.

Aidha mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania Mfaume Juma amewaomba wakulima kutohamisha udongo kutoka sehemu ambayo imeonekana na ugonjwa huo na kupeleka sehemu nyingine.

No comments:

Post a Comment