Tuesday 26 April 2016

Wawekezaji Kutoka Urusi kuwasili nchini Kesho


inv
Wafanyabiashara pamoja na wawekezaji kutoka Urusi wakiongozwa na waziri wa Viwanda wa Urusi Denis Matroff wanatarajia kuingia nchini kesho kwa ajili ya kutembelea na kuangalia fursa ya Uwekezaji katika nyanja mbali mbali zikiwemo za madini,Gesi,kilimo pamoja na Nishati.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm katibu mkuu wizara ya Viwanda na Biashara Prof Adolf Mkenda amesema wafanyabiashara hao pia wataangalia katika uwekezaji wa Usafiri wa anga,viwanda pamoja na kilimo kutokana na Urusi kupiga hatua kubwa katika sayansi na mapinduzi ya Viwanda.

Mmoja wa wawakilishi wa wawekezaji hao kutoka Kampuni ya Usafirishaji ya B2B Export ya nchini Urusi Ektaria Dyachenko amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye fursa kubwa za uwekezaji huku pia akieleza nia ya Urusi katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara.

No comments:

Post a Comment