Thursday 21 April 2016

Waziri Kitwanga Asema haya kuhusu Zitto Kabwe

Waziri Kitwanga amekanusha kuwa hausiki na suala hilo, alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Drive kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa hana mamlaka yoyote ya kuwatuma vina hao kufanya hivyo, kwani yeye ni kiongozi wa kawaida kama wengine.

“Mimi jamani nina mamlaka gani na Umoja wa Vijana waweze kunifacilitate mimi, mimi ni kiongozi tu wa kawaida, nina mamlaka gani ya kuwaambia umoja wa vijana? Ajue kwamba mimi sina mamlaka". Amesema Kitwanga
Waziri Kitwanga aliendelea kusema kuwa hata tuhuma anazompa hajui chochote kinachoendelea, kwani ana jukumu zito la kuhakikisha nchi inakuwa salama, na hata hivyo hapendi mambo ya kiswahili.
“Mimi sijui kinachoendelea, mimi sijui anachozungumza, natumiwa kwenye meseji na sitaki kusoma, sijaona na sitaki kuona kwa sababu watani-divert kwenye kazi zangu za msingi, madawa ya kulevya kuyaondoa nchini tanzania, majambazi kuyaondoa nchini na kuhakikisha nchi yetu iko salama, mimi mengine yote mnayozungumza ya uswahi swahili huko siyahitaji, mimi ni mtenda kazi”. Amesema Waziri Kitwanga.
Pia Waziri Kitwanga amewataka Watanzania au mtu yeyote mwenye mashaka na mali zake, aende kufuatilia Tume ya Maadili kwani ameorodhesha mali zake zote, pamoja na makampuni ambayo anashea nayo, ambayo yamesajiliwa na Brela.
“Mimi ninaongozwa na masharti ya kazi, mimi nina share holding kwenye makampuni mengi, lakini ningewashauri watanzania pamoja na huyo ambaye amewaambia, waende tume ya maadili, mali zangu pamoja na kampuni ambazo mimi nina share holding, nimeviorodhesha waende , na wakishaenda kampuni zote zimesajiliwa na brela, waende brela, mimi sihitaji kushughulikia mambo ambayo hayanihusu, nahitaji kutumikia watanzania kwa kazi niliyopewa na Rais John Pombe Magufuli, kila mtu afanye kazi yake”. Amesema Waziri Kitwanga.

Alichokiandika Zitto Kabwe kuhusu Waziri Kitwanga kutumia watu kumchafua.

No comments:

Post a Comment