Thursday 14 April 2016

Waziri Simbachawene afuta bodi ya soko la Machinga Complex Dar es salaam

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, George Simbachawene akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda nyaraka za jengo la Machinga Complex baada ya kuvunja bodi ya jengo hilo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI GEORGE SIMBACHAWENE ameifuta bodi ya soko la MACHINGA COMPLEX la jijini DAR ES SALAAM na kuwasimamisha kazi watumishi wanaosimamia uendeshaji wa soko hilo kwa kushindwa kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo wadogo.


Waziri SIMBACHAWENE ametoa tamko hilo wakati akihutubia mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini uliofanyika jijini DAR ES SALAAM na kumtaka Mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA kuweka utaratibu utakaowanufaisha wafanyabiashara wadogo wadogo.
Waziri SIMBACHAWENE  amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuwa walezi wa Jumuiya za wafanyabiashara ili kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.

No comments:

Post a Comment