Saturday, 23 April 2016

Winga wa Azam FC Farid awasili Madrid, Hispania kwa majaribio



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Winga wa Azam FC, Farid Mussa amewasili nchini Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu za La Liga.
Akizungumza kutoka Madrid, Hispania, Farid amesema leo ndiyo atajua ratiba nzima ya mazoezi.
Farid atakuwa nchini humo kwa muda wa mwezi mmoja akifanya majaribio klabu za Union Deportiva Las Palmas, maarufu kama Las Palmas yenye maskani yake Las Palmas de Gran Canaria na Athletic ya Bilbao.
Farid amewasili Hispania akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne.

No comments:

Post a Comment