Saturday 23 April 2016

Vyuo binafsi wataka utafiti zaidi ada elekezi nchini

Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi nchini Tanzania Profesa Eustella Balalusesa amesema kuwa suala la ada elekezi si kitu kigeni nchini Tanzania ila kwa hivi sasa serikali inalenga zaidi kufanya mabadiliko ya kuendana na mabadiliko ya maisha yaliyopo kwa hivi sasa.

Ametoa kauli hiyo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na umoja wa wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Binafsi TAMONGOSCO kwa lengo la kujadili kwa pamoja jinsi ya kufanya tathmini ya gharama halisi za kumuelimisha mtoto kwa elimu za sekondali na elimu ya msingi na wawezse kufikia mapendekezo ya ada elekezi ambayo haitamuumiza mzazi wala mmiliki wa shule.
Aidha kwa upande wake Katibu mkuu wa TAMONGOSCO Benjamin Mkonya ameiomba serikali kufanya utafiti wa kina na yakinifu katika kupanga ada elekezi kwa kupambanua vizuri huduma zinazotolewa ,aina ya walimu waliopo na upatikanaji wa vifaa vya mafunzo.

No comments:

Post a Comment