Thursday 12 May 2016

Baada ya kiapo Rais Museveni kuahidi makubwa tazama hapa.

Rais Museveni ambapo wananchi wengi pamoja na wageni wengi kutoka nje ya taifa hilo wamejitokeza kushiriki sherehe za kuapishwa kwake katika uwanja wa Kololo.

Akizungumza mara baada ya kula Kiapo Museveni amesema uchumi wa nchi hiyo umekuwa sana lakini tatizo ni kwamba tunanunua vitu vingi kutoka nje na tunauza vichache pia kucheleweshwa kuchukuliwa kwa hatua kwa watu wanaofisadi taifa hilo kunawaudhi raia na kutowavutia wawekezaji hivyo atahakikisha vitendo hivyo vinakoma.

Kuhusu suala la amani Museveni amesema hakuna mtu anayeweza kuharibu usalama wa Uganda na kuwataka viongozi wenzake wa Afrika kuimarisha usalama wa Somalia na Congo.
Aidha Rais huyo amekosoa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu kuwa ni bodi isiyo na maana.''Tuliunga mkono ICC tukidhani ni mahakama nzuri lakini baadaye tukagundua ni mahakama yenye watu wasio na maana''. Museveni ameyasema hayo baada ya kuthamini uwepo wa Rais wa Sudan Omar el Bashir.

Rais Museveni atatawala taifa hilo kwa muhula wa tano mfulilizo ambapo uchaguzi mwingine utaitishwa mwaka 2021 baada ya kumaliza kipindi cha miaka 5.

viongozi wa mataifa 14 kutoka Afrika na wageni wengine mashuhuri, wamehudhuria akiwemo Rais wa Tanzania John Magufuli, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Rais wa Sudani Kusini Salvar Kiir, Rais wa Sudan Omar el Bashir, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na viongozi wengine

No comments:

Post a Comment