Thursday, 12 May 2016

UVCCM Mwanza kugombania eneo la mapumziko mwalimu Nyerere na wakazi wa Igoma.


Enezo la mapumziko ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, limegubikwa na mgogoro kati ya wakazi wa kata ya Igoma dhidi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kuhusu uhalali wa umiliki wa eneo hilo.


Ni mvutano wa miaka kadhaa sasa tangu mgogoro huo ulipoanza kurindima, ambapo wakazi wa eneo hilo linalofahamika kama Mtaa wa Nyerere, wamedai kuwa mtaa huo upo chini ya umiliki wao tangu miaka ya 70, wakati wa harakati za Azimio la Arusha.Ingawa wakazi hao wamethibitisha kuwa wanao uhalali wa kuendelea kuishi katika eneo hilo, lakini Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza umeyapinga madai hayo.

Wakati mvutano huo ukiendelea, Mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere kata ya Igoma John Manoni, akatoa ufafanuzi juu ya mgogoro huo.

Tangu mgogoro huo ulipoanza kurindima miaka ya 70 hadi sasa, umesababisha Wakazi wa mtaa huo kushindwa kuliendeleza eneo hilo, huku wakiiomba Serikali kuingilia kati, ili kutatua mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment