Thursday 12 May 2016

Elimu juu ya matumizi ya mabasi yaendayo kasi yafikia hapa jijini Dar es salaam.

DART
Ikiwa ni siku ya tatu tangu mabasi yaendayo haraka yaanze kutoa huduma bure jijini dar es salaam wananchi wameonekana kupata uelewa juu huduma hiyo ikiwemo namna ya kuingia katika vituo vya kusubiria usafiri huo pamoja na matumizi ya kadi na risiti mahali zinapopatikana.

Akitoa elimu kwa wananchi Salim Chuma amesema kadi hiyo itatumiwa na mwenye kadi tu na si mtu mwingine hivyo ametoa onyo kwa mtu yoyote kuiba ama kutumia kadi isiyokuwa yake kuwa ataibainika na mashine zinazotambua kadi hizo wakati wa kuingia na kutoka katika kituo ambapo ina milio mitatu ikiwemo mlio unaonyesha salio, hamna salio na kadi sio yako.

Abiria wanaotumia usafiri huo wamesema kwa sasa wameanza kuelewa namna mabasi hayo yanavyofanya kazi ikiwemo baadhi ya mabasi kutosimama vituo vyote ingawa wameomba elimu zaidi iendelee kutolewa.

Mabasi yameguka kilio kwa makondakta wa daladala wanaotumia barabara ya morogoro ambao wanadai kuwa kwa sasa biashara imekuwa ngumu.

No comments:

Post a Comment