Thursday, 19 May 2016

Agizo la Rais Dk. Magufuli la kukabiliana na uhaba wa madawati lafikia hapa jijini Mwanza

 
Katika kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini,
Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imefanikiwa kupunguza tatizo hilo, baada ya kutengeneza Madawati elfu 12,779 kati ya Madawati 22,061 yanayohitajika.

Juni 30 mwaka huu ndio kilele cha utekelezaji wa agizo hilo, ili kuwaepusha wanafunzi wa shule za msingi nchini kukaa sakafuni, ambapo wilaya ya Misungwi mkoani hapa imekuwa moja kati ya wilaya zinazotekeleza vyema zoezi hilo, baada ya kubaki na deni la Madawati elfu 9,282, ili kukamilisha zoezi hilo.

Kabla ya utekelezaji huo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, ilikuwa na jumla ya Madawati 12,536.

Kutokana na mafanikio hayo, Afisa elimu wa Halmashauri hiyo Ephrahim Majinge, amesema wadau mbalimbali bado wanaendelea kujitokeza, ili kukamilisha zoezi hilo.

Kisha baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wakaeleza jinsi walivyoguswa na zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment