Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA imefanya Ukaguzi katika machinjio ya
Vingunguti Jijini dsm ili kujiridhisha na Hali ya
Usafi na Ukarabati wa Miundombinu katika machinjio hayo ili kutoa kibali cha kuweza kuendelea kufanya shughuli za Uchinjaji na Uuzaji wa nyama katika machinjio hayo.
Afisa Mkaguzi wa Mamlaka hiyo Dr.Jerome Kiwanga akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi huo amesema pamoja na kufanyika kwa marekebisho makubwa bado kuna maeneo zaidi yanayohitajika kufanyiwa Ukarabati.
Aidha Dr.Kiwanga amebainisha baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni pamoja na kutokuwapo kwa zizi la kuwatunza wanyama wagonjwa na eneo la kuhifadhia nyama inayotaka kupelekwa katika mabucha.
Wakati zoezi hilo likifanyika makundi ya Vijana na wafanyabiashara katika eneo hilo walionekana kutoridhishwa na taarifa hizo kwa madai kuwa wamekaa kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu bila kufanya shughuli zozote hali iliyosababisha kuingia katika mgogoro na taasisi za fedha kutokana na wengi wao kukopa kwa ajili ya kuendesha biashara zao.

No comments:
Post a Comment